RATIBA YA LOWASSA MTIHANI KWA DK MAGUFULI


Ratiba za kampeni za wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoonekana kuchuana vikali, Edward Lowassa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeibua mgongano.
Hali hiyo imelalamikiwa na CCM ambayo imeitupia lawama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwamba imeshirikiana na Chadema kupanga njama hizo.
Kufuatia hali hiyo, jana Nec iliingilia kati na kuitisha kikao cha kupitia upya ratiba za kampeni za vyama.
Kampeni za vyama ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, zilianza rasmi Agosti 22, mwaka huu baada ya Nec kufanya uteuzi wa wagombea.
Kwa mujibu wa taratibu na sheria, kabla ya kampeni kuanza vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi hutakiwa kuwasilisha ratiba zao Nec na baadaye tume hiyo hupanga ratiba ya nchi nzima kujumuisha vyama vyote.
Hata hivyo, kampeni za wagombea wa vyama hivyo mikoani zinaonyesha kuwa wamekuwa wakifuatiliana hususani Lowassa kwenda maeneo ambayo Magufuli anatoka kujinadi kwa wapigakura.
Lowassa alianza ziara yake mikoani Agosti 30, mwaka huu katika mkoa wa Iringa ambako alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mufindi, Kilolo na Iringa mjini.
Baadaye aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Njombe ambako alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Makambako na Njombe mjini.
Kwa upande wake, Dk. Magufuli alitangulia kufanya ziara katika mkoa wa Njombe na kufanya mikutano katika jimbo la Njombe mjini ambako Lowassa alifanyie mkutano eneo hilo hilo.
Majimbo mengine aliyotembelea ni Makete mjini na Wanging’ombe.
MKOA WA RUVUMA
Dk. Magufuli alitangulia kufanya ziara kwa kufanya mikutano katika majimbo ya Madaba, Nyasa, Mbinga mjini, Peramiho na kufunga pazia Songea mjini katika uwanja wa Majimaji.
Kwa upande wake, Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika jimbo la Madaba, Songea mjini na Tunduru.
MKOA WA KATAVI
Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Nkasi, Mpanda mjini na Namanyele.
Kwa upande wake, Magufuli ambaye alikuwa wa kwanza kuwasili mkoani humo, alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mpanda vijijini na Mpanda mjini.
MKOA WA RUKWA
Dk. Magufuli alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Milele, Nkasi, Kalambo na Kwela.
MKOA WA MOROGORO
Dk. Magufuli alifanya mkutano wa kwanza wa kampeni jimbo la Mahenge, Malinyi, Ifakara na Morogoro mjini.
WALIVYOGONGANA NJOMBE, IRINGA.
Magufuli aliingia Njombe na kufanya mikutano katika jimbo la Njombe Mjini, Makete Mjini na Wang’ing’ombe.
Lowassa alianza ziara yake mikoani Agosti 30. Akatua Iringa katika majimbo ya Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini. Kisha akatua Njombe alikotoka Magufuli na kuhutubia Makambako na Njombe mjini.
RUVUMA
Dk. Magufuli aliingia Ruvuma na kufanya mikutano Madaba, Nyasa, Mbinga Mjini, Peramiho na kumalizia Songea Mjini.
Lowassa naye akatua na kufanya mikutano ya kampeni alikopita Magufuli katika majimbo ya Madaba, Songea Mjini na kisha akafanya hivyo Tunduru.
KATAVI
Magufuli aifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mpanda Vijijini na Mpanda Mjini.
Siku chache baadaye, Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Nkasi, Mpanda Mjini na Namanyele.
RUKWA
Dk. Magufuli alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mlele, Nkasi, Kalambo na Kwela.
Hata hivyo, Lowassa hajafika katika majimbo ya mkoa huo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA