RAIS NKURUNZINZA ATUMIA BAISKELI KUFIKA KWENYE KITUO CHA KUPIGA KURA YA WABUNGE !!



 
 



Jana Juni 29 vyomba mbalimbali vya habari vilikuwa na taarifa ya kuhusu kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge nchini Burundi.

Uchaguzi ambao ulifanyika, huku vyama vya upinzani na Umoja wa Afrika wakiwa  wamesusia uchaguzi huo.

Yote hayo yanafuatiwa na ile hali ya wananchi wa nchi hiyo kumpinga Rais Pierre Nkurunzinza kugombea kwa mara ya tatu nafasi ya urais.

Miongoni mwa watu waliojitoketa jana kupiga kura katika kuchagua wabunge alikuwa ni pamoja na Risi Nkurunzinza mwenyewe ambaye alifika kwenye kituo cha kupigia kura kwa njia ya usafiri wa baiskeli.

Zipo picha zake hapa chini unaweza kuzitazama..
Rais Pierre Nkurunzinza akiwasili kwenye kituo cha kupigia kura
Rais Pierre Nkurunzinza akiwa katika foleni ya kuelekea kupiga kura
Rais Pierre  Nkurunzinza akitumbukiza kura yake ndani ya sanduku la kura
Wanausalama nao hawakuwa mbali na kituo cha kupigia kura na walikuwa wamejitayarisha


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA