MASIKINI AUNT EZEKIEL AKIRI AIBU YA KUZAA NJE YA NDOA YAKE
Aunt Ezekiel na mume wake Moses Iyobo wakifurahia na mtoto wao.
Mkali wa sinema za Kibongo Aunt Ezekiel akiwa na wafanyakazi wa Globalpublishers walipomtembelea kumuona mtoto wake.
Makubwa! Aunt Ezekiel
ameweka wazi kinachotafsirika kuwa ni kuzaa nje ya ndoa huku akishikilia
alichokiita ‘hayo ni mambo yake binafsi’, Ijumaa Wikienda
liligaragazana naye kwa maswali.
Akizungumza kwa njia ya
simu na ‘kijumbe’ wetu wikiendi iliyopita, mkali huyo wa sinema za
Kibongo, alisema kamwe hapendi kuulizwa masuala ya ndoa yake.
Aunt alisema suala hilo
ni la kifamilia na kwamba yeye ndiye mwenye siri ya nani baba wa mtoto
huku akishindwa kukubali kama ni Sunday Demonte ambaye ni mumewe wa
ndoa, ndiye baba wa mwanaye Cookie.
“Mume wangu anapaswa
anisikilize mimi, hakuna mahali niliwahi kusema kuwa mtoto huyu ni wa
Iyobo (anayetajwa kuwa ni mpenzi wake), ni kweli nimepiga picha na Iyobo
tukiwa na mtoto, lakini mtu yeyote anaweza kuja nyumbani, hata wewe
(mwandishi), tukapiga picha nikiwa na mwanangu.
“Kuhusu Demonte, huyo ni
mtu wangu, siwezi kusema mtoto ni wa kwake na siwezi kusema si wa
kwake, ni mambo yangu binafsi, kama yeye (Demonte) akiamua kufuata
maneno ya watu, sawa lakini ni bora anisikilize mimi mkewe,” alisema.
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida, Aunt alimlalamikia mwandishi wetu kwa maswali mengi na mazito
yaliyosababisha kukaukiwa maziwa kwenye matiti yake na kwamba kwa wakati
ule hakujua mwanaye Cookie angenyonya nini.
Maoni
Chapisha Maoni