Machapisho

KUTOKA BUNGENI: Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Rasmi Mwaka 2020

Picha
Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma. “Ili kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka 2016/2017 kama ifuatavyo”– 1. Septemba 2016 – Februari 2017. Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma; 2. Machi 2017 – Agosti 2017. Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma. 3. Septemba 20...

Malawi Yadai Kuishtaki Tanzania Kwenye Umoja wa Afrika(AU)

Picha
Foreign Affairs and International Cooperation minister Francis Katsaira said Tanzania has released a new Lake Malawi map which shows the east African country has taken a chunk of Lake Malawi, which is potentially rich in oil and gas.. “We have already reported them to the African Union and very soon we will be reporting them to Comesa and Sadc,” he said. Kasaira said Tanzanian authorities have threatened to beat up and arrest Malawians who will disregard the new map. The old map, drawn up by Germany and Britain gives the whole Lake Malawi, except a small part to Malawi. Tanzania has taken much interest in the lake after oil was discovered in the lake popularly known as lake of stars. Katsaira said both Malawi and Tanzania were supposed not to interfere with the Lake Malawi issue as the matter was with the African Union and a mediation team. He therefore said the government is waiting for a response from Tanzsnia on the proposal fo...

Namanga: Edward Lowassa asimamishwa na wananchi wamweleze ugumu wa maisha

Picha
Mh Edward Lowassa Mjumbe wa kamati kuu wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na Chama kikuu cha Upinzani TANZANIA na Waziri Mkuu mstaafu amesimamishwa na Wananchi wa Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya .  Wananchi wamemueleza Ugumu na ukali wa Maisha walionayo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha mpakani hapo leo hii akiwa safarini Toka Nairobi Kenya alipokwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu Ole Ntimama.

Gavana BOT Afichua Siri ya Kilio Cha Fedha Kupotea Mtaani

Picha
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo. “Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu. Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki z...

Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta

Picha
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda. Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi. Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa. Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utaw...

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni leo 18 Aug 2016

Picha
Hapa Chini Nimekuwekea Nafasi za kazi Mbali Mbali zilizotangazwa leo katika Magazeti na Mitandaoni, Bonyeza Links Job Opportunities at Acacia Mining, Application Deadline: 26 Aug 2016 Job Opportunity at Sun Share, Application Deadline: 24 Aug 2016 Job Opportunity at Serengeti Breweries Limited (SBL), Serengeti Breweries Limited (SBL) Job Opportunity at Tanzania Postal Bank (TPB), Application Deadline: 25 Aug 2016 Job Opportunity at Four Seasons Hotels and Resorts, Application Deadline: 22 Aug 2016 Job Opportunity at 7Skyee Consultancy Private Limited, General Manager - Treasury Job Opportunity at 7Skyee Consultancy Private Limited, General Manager (Accounts) Nafasi Zingine Unaweza Kutembelea:  WWW.AJIRAYAKO.COM

Ni Kosa Kumwangalia Mwanamke Kwa Sekunde 14 Nchini India

Picha
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India. Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani. Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda. Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake. ”Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”,alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi. Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii. Source:BBC