Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta


Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda.

Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi.

Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa.

Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utawala wa sheria uzingatiwe, tutaandamana kutetea haki yetu ya kikatiba kufanya mikutano.

Amesema kwamba kwa sababu wamejiandaa kutupiga, nasi tumejiandaa kwa kila kitu, kwamba tunajua tarehe moja siyo siku ya harusi, kwamba tarehe moja tumejiandaa kwenda jela ama kuawa.

Tunajua tunakwenda kukumbana na polisi wakiwa na silaha na mabomu lakini tumejiandaa.

Kama Mauti imepoteza utukufu wake kwangu, hakuna statement yoyote inayoweza kurudisha Arusha kuandamana.

Amemuonya Mwigulu apime kauli zake kabla hajaitoa.

Lema amesema madai ya chadema ni madai ya msingi na endapo madai yake yatapuuzwa nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.

Mh Lema amesema hatuandamani bei ya konyagi ipungue, bali tunaandamana utawala wa sheria katika taifa hili uzingatiwe.

Kama leo haturuhusiwi kufanya mikutano ya hadhara kwasababu rais amesema, iko siku misikitini ama makanisani itafungwa kwasababu rais amesema. Hii vita ni ya kila mtu katika taifa hili, siyo vita ya chadema

Nitakuja kumalizia baadaye kidogo nimalizie natafuta namna ya kuiweka clip hapa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA