Uganda: Polisi Esther Naganda anayedaiwa kupigwa adai Shilingi milioni 200
Afisa wa polisi mwanamke wa Uganda anayedaiwa kushambuliwa na Meja Generali Matayo Kyaligonza na walinzi wake wawili amefika mahakamani kuomba apewe fidia ya shilingi za Uganda milioni 200.
Mwezi Februari video inayodaiwa kuwa ni ya Afisa Namaganda akiburuzwa na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa walikuwa ni walizi wa Meja Generali Matayo Kyaligonza iliibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda na nje ya nchi hiyo.
Awali walinzi wa Meja Jenerali Kyaligonza walikamatwa kuhusiana na kisa hicho
Akiwa Mahakamani Bi Esther Namaganda- ambaye ni Afisa wa usalama barabarani , anataka pia alipwe shilingi milioni 1 kama gharama ya uharibifu aliotendewa , Shilingi milioni 200 kama jenerali na adhabu kwa kosa alilotendewa la kuumizwa, kisaikolojia na kimwili na kusababishiwa aibu aliyopata wakati alipodaiwa kupigwa na mkuuu wake mwenye umri wa miaka 73-ambaye pia ni balozi wa Uganda nchini Burundi.
Februari 24, 2019 Bi Namaganda alisema kuwa wakati alipokuwa kazini kwenye kituo cha udhibiti wa kasi ya magari yanayotoka Kampala kuelekea kitongoji cha Mukono kwa usaidizi wa maafisa wenzake wawili wa polisi - Solomon Nkubito na William Ariku- ghafla gari linalomilikiwa na Maja Jenerali Kyaligonza lililokuwa likisafiri kutoka Kampala lilimkaribia na kuonyesha kuwa lilikuwa linaelekea Kampala ikionyesha kuwa dereva alikuwa anageuza gari kurudi kampala, jambo lililokuwa ni kinyume cha sheria. Aidha ameelezea kuwa dereva wa mshitakiwa aliendelea kuvunja sheria kwa kugeuza gari lake (u-turn) jambo lililomfanya amuonyeshe ishara ya kugeuka ipasavyo kwenye kituo cha mafuta cha Kobil lakini alikaidi.
" Lakini jambo lililonishutua ni kwamba , walinzi wa Meja Jenerali waliruka nje ya gari na kumvuta shati upande wa kooni (kumkwida) huku wakimvuta nje ya barabarahuku Balozi huyo wa Burundi akishuhudia," Alisema Bi Namaganda mahakamani.
Maoni
Chapisha Maoni