Kenya: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu akamatwa kwa kuingia Ikulu kinyume cha sheria
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, anauguza majeraha katika katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta baada ya kupigwa risasi na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaopiga doria kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.Siku ya Jumapili Jioni Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa ataingia Ikulu.
Tomorrow I attack State House. God has sent me to execute judgement on every thief and every partner of a thief,” -
Kibet Bera pic.twitter.com/3qIzntofat
— ktn (@KTNKenya) 11 Juni 2019
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo Kisa hicho kilitokea Jumatatu na mshukiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa na kusajiliwa katika Kitabu cha Matukio nambari 39 kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.
'Tunachukua fursa hii kukumbusha umma kwamba Ikulu ni mahali polipotengwa kuwa chini ya ulinzi mkali kwa mujibu wa Sheria ya Maeneo Yanayolindwa (Protected Areas Act). Kwa sababu hiyo, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia Ikulu pasipo na ruhusa ya mamlaka yenye jukumu hilo.'' alisema Bi Kanze
Maoni
Chapisha Maoni