Ali Kiba afunga ndoa na mpenziwe wa Kenya
Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya.
Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.
Mwanamuziki huyo wa wimbo wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake.
Ni watu wachache pekee walioalikwa katika harusi hiyo iliodaiwa kufanyika kisiri.
- Zari: Nimeachana na Diamond
- Diamond akiri kuwa na mtoto nje ya ndoa
- Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
Duru zimearifu kwamba sherehe nyengine ya kukata na shoka inatarajiwa kufanyika Aprili 26 mjini Dar es Salaam.
Maoni
Chapisha Maoni