CRISTIANO RONALDO MMMH!
Cristiano Ronaldo 'anataka kuihama' Real Madrid juu ya kodi 16 Juni 2017 Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Cristiano Ronaldo amekuwa Real Madrid kwa miaka minane Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekereka sana baada ya tuhumiwa kwamba alifanya ulaghai wakati wa ulipaji ushuru na anataka kuihama klabu hiyo, duru zimeiambia BBC. Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghari kutolipa mamilioni ya ushuru. Amekanusha tuhuma hizo. "Anahisi kwamba amekuwa mkweli, ana sifa nzuri na alifanya kila kitu ipasavyo," ameongeza mdokezi. Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo ya Madrid una kifungu cha euro bilioni moja (£874.88m), ambacho kinafaa kufikishwa ndipo afunguliwe kutoka kwa mkataba...