Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

Pep Guardiola Atumika Kumvuta Messi Etihad Stadium

Picha
Klabu ya Manchester City inaamini ujio wa kocha Pep Guardiola, huenda ukamshawishi mshambuliaji hatari kutoka nchini Argentina na FC Barcelona, Lionen Adres Leo Messi, kujiunga na klabu hiyo ya Etihad Stadium. Licha ya kudhibitisha kwake juu ya kutokuwa na mpango wa kuihama FC Barcelona inaamini kwamba ujio wa meneja huyo kutoka nchini Hispania, utamvutia ikizingatia kwamba amekuwa na kashfa ya ukwepaji wa kodi. Hata hivyo Manchester City, italazimika kutoa kitita kikubwa cha fedha endapo itahihitaji kwa dhati huduma ya mshambuliaji huyo aliyetengeneza muunganiko mzuri wachezaji wengine huko Camp Nou akiwepo Luis Suarez na Neymar. Lionel Messi aliwahi kukaririwa akikana kuwa na nia ya kuihama klabu ya Barcelona yenye maskani yake Katulanya

SAMATTA AING’ARISHA STARS UGENINI...CHAD 0-1 TAIFA STAA

Picha
Mbwana Samatta akivaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza, amekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Chad kwenye mchezo wa Group G kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mwaka 2017 nchini Gabon. Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo. Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria ‘The Super Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa. Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Msimamo wa Group G unaongowa na Misri yenye pointi 6 ikifatiwa na Nigeria na Tanzania zenye pointi 4 ...

Mkuu wa Wilaya Lucy Mayenga Aihofia Kasi ya Magufuli..Ajisalimisha na Kumuomba Rais Asimchague Tena Ukuu wa Wiliya

Picha
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizos...

LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH

Picha
Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Lady Jaydee amefunguka kuhusiana na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gadner G Habash. Aliulizwa swali hilo na mtangazaji Sam Misago katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa. “Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama mimi kama Jaydee na si vinginevyo,”alisema Jaydee. Msanii huyo ameibuka tena na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndindindi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari. CHANZO na Bongo5.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKABIDHIWA TUNZO YA MSANII BORA AFRIKA

Picha
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wasanii wa Film wa hapa Nchini baada ya kukabidhiwa    Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA)    na Tunzo ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria, hafla hiyo iliyofanyika leo March 14,2016     Oysterbay Dar es salaam.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA) iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Elizabeth Michael (Lulu) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar es salaam leo March 14,2016.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Single Mtambalike (RICHIE) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar...

Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kukata Jina Lake na Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa

Picha
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli  alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro. Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia nyadhifa hiyo. “Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii. “Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro. Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa kati...

HOTEL NZURI NA KUBWA ZAIDI DUNIANI ILIYOJENGWA KATIKATI YA BAHARI(+MAPICHAZ)

Picha

Forbes rates Dangote richer than Trump, Abramovich, Oprah put together

Picha
Aliko Dangote, president of Dangote group, is now richer than Donald Trump, Republican front runner; Roman Abramovich, owner of Chealsea football club and Oprah Winfrey, the richest black woman, put together. Dangote, who came in at the 51st position of the 2016 ranking by Forbes Magazine, is also richer than the combination of all other Nigerians who made the list. Despite losing $300 million from $15.7 billion (N3.1 trillion) to about $15.4 billion, (N3.05 trillion) in the latest rankings, Dangote remains the richest black billionaire anywhere on the planet. At $15.4 billion, the 58-year-old is richer than Abramovich ($7.6 billion), Oprah ($6.2 billion) and Trump $4.5 billion. The Nigerians who made the list are Mike Adenuga ($10 billion), Femi Otedola ($1.8 billion), Folorunsho Alakija ($1.6 billion) and Abdulsamad Rabiu ($1.1 billion), who came in at 103, 1,011, 1,121 and 1,577 respectively. Bill Gates remains the richest person in the world with a net ...

Breaking News: Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26....Kati Yao 13 ni Wapya, 7 Wamebakizwa na 5 Wamehamishwa

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe. Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.   Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo; Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa...

HUYU NDO MTANZANIA KINARA WA DAWA ZA KULEVYA ALIYE WEKEWA VIKWAZO NA MAREKANI

Picha
Ni yule mtuhumiwa maarufu wa kusapply poda duniani... Kingpin Act Designations; Sudan Designation Removal 3/9/2016 OFFICE OF FOREIGN ASSETS CONTROL Specially Designated Nationals List Update The following individual has been added to OFAC's SDN List: HASSAN, Ali Khatib Haji (a.k.a. ALEX, Maiko Joseph; a.k.a. HAJI, Ali Khatib; a.k.a. HAJI, Ali Khatibu; a.k.a. SHAKUR, Abdallah; a.k.a. "SHIKUBA"; a.k.a. "SHKUBA"); DOB 05 Jun 1970; alt. DOB 01 Jan 1963; alt. DOB 08 Jun 1970; POB Zanzibar, Tanzania; alt. POB Dar es Salaam, Tanzania; nationality Tanzania; citizen Tanzania; Gender Male; Passport AB269600 (Tanzania); alt. Passport AB360821 (Tanzania); alt. Passport AB564505 (Tanzania); alt. Passport A0389018 (Tanzania); alt. Passport AB179561 (Tanzania); alt. Passport A0010167 (Tanzania) (individual) [SDNTK]. The following entity has been added to OFAC's SDN List: HASSAN DRUG TRAFFICKING ORGANIZATION (a.k.a. HASSAN DTO;...

Ukitaka Kupata Msongo wa Mawazo Mpaka ufe oa Hawa Wafuatao

Picha
1. Mama mwenye mtoto/watoto aliyeachika akiwa kwenye ndoa 2. Mwanamke aliyeachika ndani ya ndoa 3. Mwanamke yupo karibu mitandao yote ya kijamii, hakuna habari ya kimbea yeye anapitwa (Tena siku hizi WhatsApp wanawake hasa akina dada wana magroup, hadi migegedo ya saizi mbalimbali wanatumiana) 4. Mdada aliyeenda umri halafu anaishi gheto ( Hawa mara nyingi wamekubuhu, hadi wanaume wakwere wanawakwepa, wadada hawa hujifanya social, wana msururu wa marafiki wa kiume, mara nyingi hit and run kwao ni kawaida) 5. Mdada unayemtongoza siku moja, ya pili au ya tatu ukimwita kwako, anajileta. Kumbuka wewe sio wa kwanza kumtongoza, wewe labda ni wa hamsini.

GARI KALI TANO AMBAZO HUWEZI KUZIONA BONGO "PICHA

Picha

RAIS MAGUFULI AMTUMBUA BALOZI Ombeni Sefue

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.  Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine. Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi  wa Mawasiliano,  IKULU - Dar es Salaam 06March,201 Katibu Mkuu Kiongozi Mpya, Balozi John William Kijazi

Zifahamu simu zitakazo shindwa kutumia mtandao wa WhatsApp ifikapo Desemba 2016

Picha
Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1. Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.” WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016. Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android. Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia. “Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema. Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa: Android 2.1 and Android 2.2 Blackberry OS 7 and earlier ...

Wassira Amvaa January Makamba...... Asema Huenda Yeye ndo Alibebwa Tano Bora ya Urais CCM

Picha
The Choice 8 hrs ago MWANASIASA mkongwe aliyekuwa waziri katika Serikali ya awamu nne, Stephen Wasira, amemshangaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba aliposema kuwa uwajibikaji katika utawala wa awamu ya nne ulikuwa ni wa kuleana. Kauli ya Wasira imekuja siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kumnukuu Makamba akisema uwajibikaji katika Serikali ya awamu hiyo haukuwa wa kuridhisha kwasababu kulikuwa na utamaduni wa kuoneana haya, kujuana na kusitiriana. Akizungumza  katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam jana, Wasira alieleza kushangazwa na kauli hiyo ya Makamba akisema yawezekana aliyelelewa ni yeye. “Labda alilelewa yeye…kama rafiki yangu Makamba anasema kulikuwa na kuleana, mimi kwa upande wangu sikulelewa nilifanya kazi na nikatimiza wajibu wangu kama nilivyopewa na Rais. “Sasa kama aliona kulikuwa kuna kuleana mimi sijui yeye ndiye anajua maana mimi sikulelewa. Kama...

Mama yake Halima Mdee alia na serikali ya Magufuli

Picha
Mama mzazi wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mama Theresia Mdee ameilalamikia Serikali ya Awamu Ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kutokana na yanayomsibu mwanae. Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kupekuwa nyumba ya Halima Mdee, ambaye wiki hizi mbili zilikuwa chungu kwake baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi na kulazwa rumande. Mama huyo alieleza kuwa kinachofanywa na serikali dhidi ya mwanae ni uonevu wa dhahiri na kumnyima haki. “Hii serikali kwakweli tunaona kwamba haitutendei haki. Hayo yote wanayomfanyia huyu mtoto hakuyafanya. Wanamuweka ndani bila sababu, wanakuja kumsachi hakuna kitu… ni kiasi cha kumuumiza tu na kumkandamiza ili asiweze kufanya kitu,” alisema. Hata hivyo, Mama huyo alitahadhalisha kwamba vitendo hivyo vinavyofanywa dhidi ya mwanae huenda vikawa chanzo cha kumkuza zaidi, “Sasa wajue kwamba wanamtia moshi”. Mdee alishikiliwa na polisi kufuatia vurugu zilizoibuka k...

Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Picha
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi. Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa  moja, lakini  habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.  Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu  za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani  akidai bado anamtambua Josephine  kuwa ni mke wake wake halali. Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama  impatie haki  yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa. Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa  mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50. Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini la...

Hiki ndicho kilichofikiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Kahama.

Picha
.tz/media/image/kaha.jpg" /> Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka jana iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Kahama mjini Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea wa CCM Mh.Jumanne Kishimba imeendelea leo katika mahakama ya wilaya ya Kahama. Kesi hiyo  amnbayo iliendelea kuunguruma leo majira ya saa tano kamili huku wananchi waliofika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo wakiilalamikia mahakama kutoweka vipaza sauti  hali inayosababisha idadi kubwa ya wananchi waliofika kusikiliza kesi hiyo kushindwa kuelewa nini kinaendelea.   Aidha baada ya jaji Moses Mzuna kusikiliza hoja za kila upande na kuridhika na maelezo aliagiza pande zote mbili kuleta mashahidi wao ili waanze kutoa ushahidi na kuahirisha kesi hadi kesho siku ya jumatano tar.02/03 ambapo kesi itaendelea.