MAHUJAJI WA 5 KUTOKEA TANZANIA WATHIBITISHWA KUFA HUKO MAKKA
WATU wasiopungua 700 wamekufa, huku wengine 816 wakijeruhiwa jana jirani na mji Mtakatifu wa Makka walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya nguzo muhimu katika Imani ya dini ya Kiislamu.Kwa mujibu wa Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya mahujaji 2,000,000 waliokwenda Saudi Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh Abu Bakari Zuberi Mufti wa Tanzania, kwa vyombo vya habari amesema tayari wamethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine wanne ni Watanzania.Amesema Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni, Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla. Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati wakiandaa taarifa hii ambapo raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Fatuma Mohammed Jama.Kuna ...