KUMEKUCHA CCM,MKAPA,MWINYI WAJITOSA "KUCHINJA" MAJINA YA WATAKA URAIS CCM,SOMA HAPO KUJUA
Zikiwa zimebaki siku 9 kabla ya kamati kuu ya chama mapinduzi CCM akijakutana kwa ajili ya “kufyeka” majina 37 kati ya 42 ya makada wake waliojitokeza na kuwania Urais ndani ya chama hicho,sasa jukumu lingine lawaangukia viongozi wastaafu wa chama hicho. Viongozi hao ambao ni marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa ambao wote kwa pamoja wataunda Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya kikao wakati wowote wiki hii kujadili mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho. Taarifa kutoka chanzo kimoja ndani ya CCM kimeeleza kuwa Mwinyi, Mkapa na wazee wengine wanaounda Baraza la Wazee la Ushauri, watapasua kichwa wiki hii kujadili mwenendo wa urais ikiwa ni siku chache kabla ya kufikia Julai 2, mwaka huu, inayoonyeshwa katika ratiba ya uchaguzi ya CCM kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu kwa wanaowania urais. Lengo la k...