ROSTAM AZIZI KATIKA MSIBA MKUBWA
ALIYEKUWA mbunge wa Igunga,
Rostam Aziz, (CCM), amefiwa na
baba yake Aziz Abdulrasool (73) jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu Oysterbay
jana, mtoto wa pili wa marehemu, Akram Aziz, alisema baba yake alifariki saa 12
asubuhi ikiwa ni saa mbili tu baada ya kurudishwa nchini kutoka Ufaransa
alikuwa anatibiwa.
“Baba amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
saratani,tumemrudisha nchini jana saa 10 alfajiri kutoka Ufaransa, lakini
ilipofika saa 12:30 alifariki dunia.
“Baada ya kugundulika kuwa na saratani, alianza matibabu Nchini Ufaransa na Kurudi hapa Nyumbani…Mara ya mwisho baba
alipelekwa nje miezi miwili iliyopita, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya akaomba
tumrudishe nyumbani ili awe karibu na ndugu na mafariki zake,”alisema Akram.
Marehemu alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, saa 10
jioni jijini Dar es Salaam na amewacha wajane watatu,watoto 17 na wajukuu
nane.
Maoni
Chapisha Maoni