Mchezaji wa Real Madrid Sergei Ramos amuoa Pilar Rubio
Harusi ya Sergio na Rubio iligubikwa na soka kwani nyota wengi wa soka walihudhuria Umati wa watu ulikusanyika katika kanisa kuu la Seville nchini Uhispania Jumamosi 15, Juni 2019, kushuhudia sherehe ya harusi ya mchezaji soka wa Real Madrid -Sergio Ramos aliyekuwa akifunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Pilar Rubio, ambaye ni mtangaza Televisheni. Sergio mwenye umri wa miaka 33-alikuwa nadhifu huku akiwa amevalia suti ya vipande vitatu nyeusi(three piece) iliyokuwa imeshonwa kwa mtindo wa aina yake pamoja na tai ya rangi ya kijivu iliyotulia huku bibi harusi mwenye umri wa miaka 41- akionekana kwa gauni lenye mvuto lililoiacha shingo na na mabega yake wazi kiasi cha haja. Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Marco Asensio na mkewe Sandra Garal waling'ara kwa ajili ya harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio Gauni lake refu lililogusa sakafu lililikuwa limerembeshwa kwa shanga na juu alikamilisha urembo wake kwa shela iliyowekwa nakshi. Aliamua kus...