Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani
Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha Reuters/Getty Images Image caption Muhammadu Buhari (kushoto) na Donald Trump Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la kutoka bara Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump White House atakapokutana na kiongozi huo kwa mashauriano rasmi mjini Washington baadaye leo. Marais wengine wa Afrika wamewahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, wakiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, lakini nje ya Marekani. Rais Kenyatta alikutana na Trump pambizoni mwa mkutano wa G7 nchini Italia mwezi Mei mwaka jana, naye Rais...