MAREKANI KUFANYA MAJARIBIO YA KUDUNGUA MAKOMBORA YA MASAFA MAREFU
Marekani kufanya majaribio ya kudungua kombora
Saa 4 zilizopita
Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako
Mfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini
Image caption
Mfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini
Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine.
Maafisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki ijayo.
Kumekuwa na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.
Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani anasema iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.
Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu
Korea Kaskazini yalifanyia jaribio kombora la masafa marefu
Marekani huenda isizuie makombora ya Korea
Matamshi hayo yanaonyesha wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wa Pyongyang wa kutengeza makombora mbali na mpango wake wa Kinyuklia, ambayo Korea Kaskazini inasema inahitaji kwa ulinzi wake.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa majaribio hayo yalipangwa mapema na kwamba haijibu kisa chochote.
Pentagon ilitangaza jaribio hilo wakati ambapo Korea kaskazini inatengeza kombora la masafa marefu.
Makombora ya Korea Kaskazini
Image caption
Makombora ya Korea Kaskazini
Ni mara ya kwanza Marekani kujaribu kuzuia kudungua kombora la masafa marefu ICBM.
Marekani imekuwa ikitumia kifaa cha GMD kinachowekwa ardhini kukabiliana na mashambulio ya mataifa kama vile Korea Kaskazini.
Lina uwezo wa kudungua makombora mengine lakini hawajajaribu kudungua makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Huku maafisa wa Marekani wakiamini kwamba Pyongyang ina miaka mingi ya kuweza kufanikiwa kutengeza kombora la masafa, marefu ICBM , wanaamini taifa hilo limepiga hatua.
Maoni
Chapisha Maoni