Ushauri kwa Mabinti wa Makamo Wenye Kiu na Ndoa.....


Leo nimeona nije hadharani hapa kutoa ushauri kwa mabinti wa makamo (30+yrs) ambao huenda kwa sababu za hapa na pale hawajafanikiwa kuingia kwenye ndoa wala kuwa na mahusiano yanayoashiria kuanzisha familia hivi karibuni.

Msingi wa mada yangu umetokana na mabinti kadhaa ninao kutana nao mara kwa mara maeneo mbali mbali kuwa na vilio karibu sawa.

Wakati nafanya kazi Taasisi fulani Dsm, kuna dada nilizoena nae kiasi cha kunisimulia baadhi ya mikasa ya kimahusiano na changamoto anazopitia.

Binti huyo mwenye miaka zaidi ya 30 alipitia magumu ikiwa ni pamoja na kutoa mimba kadhaa baada ya kutoona mwelekeo wa waliompachika, kuamua kugharamia mahusiano kwa kumuhudumia kila kitu mwanaume, kulazimika kubadili dini mara kadhaa kwa ajili ya mwanaume Ki uficho bila wazazi wala ndugu zake kujua.

Yote hayo aliyafanya ili kuwaridhisha wanaume angalau aitwe Mke wa fulani!! Lakini cha ajabu alikuwa anaambulia patupu

Si huyo tu, wako wengi wa namna hiyo na ambao wana visa tofauti tofauti lakini mwisho wake huishia kupata machungu na maumivu sababu ya mahusiano.

Ni kweli, ndoa ina heshima yake. Ndoa humfanya mtu aongezeke thamani katika jamii. Hilo halipingiki.

Pamoja na ukweli huo mtamu, lakini kuna ukweli mwingine ambao huenda watu hawaupendi kwamba sio wote wenye bahati ya kuwa na ndoa imara au hata hiyo ya kulega lega!! Wapo wengi wanamaisha yao mazuri na hawana hawaishi katika ndoa na wala hawajawahi kuolewa achilia mbali kutambulisha mchumba nyumbani.

Kuna mabinti wengi wanahangaika sana na wanateswa sana na mahusiano.

Unakuta Binti mzuri, mrembo, umri mkubwa tu wa kuweza kujiamlia mambo na nzuri zaidi Mungu kamjalia kazi nzuri na anauwezo wa kukabiliana na majukumu yanayohitaji pesa. Cha ajabu kutwa nzima anamaliza pesa zake kumgharamia mwanaume.

Binti huyo huyo akishika ujauzito akili hulalia upande wa kutoa eti kisa hajaolewa na anatamani sana aolewe kwani karibu rafiki zake na wadogo zake wameolewa tena kwa mbwe mbwe na michango ya harusi anatoa kila mwezi!!

Ushauri wangu ni mmoja tu, huna haja ya kuteseka wala kusononeka! Kama uwezo wa kulea unao!! Una kazi ya kukuingizia kipato, unauhakika mwanao hatokosa huduma za msingi kutoka kwako, acha kuteseka! Ruhusu moyo wako kukubali uhalisia kuwa si kila mwanamke ameandikiwa kupata watoto ndani ya ndoa. Watoto wana thamani kuliko hata hiyo ndoa unayo ng'ang'ania.

Nafahamu kuna haja za mwili za hapa na pale. Lakini ukishakuwa na maisha yako na unajitambua na kufahamu uhalisia wa maisha yako, hautashindwa kuzitimiza na kuendelea ku-control maadili ya nyumba yako!

Ni hayo tu wapwa zangu, wakuchukua achukue na wakupuuza hashikiwi fimbo!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA