RAY ABANWA KUHUSU MTOTO WA JOHARI, AFUNGUKA KUWA




SIKU chache baada ya kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi kuwa staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba na kuzaa kwa siri huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray kufunguka kuwa hahusiki kwa lolote.
 
Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
Hivi karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...
kuzungumza mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli zake.
 
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na mwanaye.
Huku akiwa amemganda Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray alikwenda mbele zaidi na kusema ni jambo la heri kujiweka mbali na watu wanaotafuta umaarufu kupitia migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa waandishi wetu na yeye kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita ‘hakuwa na mudi ya mazungumzo zaidi’.
“Achaneni na hayo mambo, sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na sipendi kabisa kuzushiwa mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa minong’ono na badala yake wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa mwanamke wa maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa natembea naye kila mahali ili kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni wapenzi wangu,” alisema Ray huku akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya ‘nadhani mmenielewa sasa’ na kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba wake.

Hivi karibuni Johari alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba ambaye alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA