Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

SALAMU za Rambirambi za Rais Magufuli Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016. Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema; "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu. Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi. Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrik...

KIMENUKA..Kura za Urais Kuhesabiwa Upya Marekani

Picha
Tume ya uchaguzi katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani limepokea ombi la kurudiwa kuhesabu kura za uchaguzi uliopita ambapo mshindi alikuwa Donald Trump aliyeshinda kwa kura chache wiki mbili zilizopita. Ombi la kurudiwa kuhesabu kura liliwasilishwa na mgombea wa urais kupitia chama cha  Green Party Jill Stein ambaye pia ametaka kura zirudiwe kuhesabiwa katika majimbo ya  Michigan na Pennsylvania. Hata hivyo ikiwa Hillary Clinton atashinda jimbo hilo hakutabadilisha matokeo ya ushindi wa Trump kwani lina kura 10 pekee za wajumbe wa uchaguzi.  Kamisheni hiyo imethibitisha kupokea maombi hayo na kuainisha kutoa maelekezo muda si mrefu.

KUFUATIA Agizo la Waziri wa Elimu Wanafanzi wa IFM Wavuliwa Majoho Katikati ya Mahafali

Picha
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kwa kuwazuia wahitimu wa ngazi ya cheti na stashahada kuvaa majoho na kofia wakati wa mahafali yao. Kitendo hicho kilitokea katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam juzi baada ya mratibu wa mahafali ya 42 ya IFM, Dk. Godwin Kaganda, kutangaza utaratibu huo licha ya wahitimu wao kuvaa majoho yao. Dk. Kaganda alisema utaratibu huo ni kwa mujibu ya miongozo iliyotolewa na Serikali kuhusu uvaaji wa majoho, ambao unataka yavaliwe na wahitimu wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea. “Wahitimu wote wa ngazi ya cheti na stashahada hamtovaa majoho wala kofia pamoja na kwamba mlishapewa awali, tunaomba radhi kwa sababu ndiyo miongozo tuliyopewa,” alisema Dk. Kaganda. Wiki iliyopita, Profesa Ndalichako  alipokuwa akiwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa, ...

Soyinka: Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa

  Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka, anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais. Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani. Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika. Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza. Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump. Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.

Trump awasili White House

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewasili katika Ikulu ya White House, kwa mujibu wa maafisa nchini Marekani. Hata hivyo aliingia akitumia mlango tofauti na kuwasili kwake hakukunaswana kamera za waandishi wa habari. Anatarajiwa kuwa kwenye mazungumzo na Rais Obama wakati huu. Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano alikishauri kikosi chake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari. Image caption Waandishi wa habari wakimsubiri Trump White House Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na ut...

Ushauri kwa Mabinti wa Makamo Wenye Kiu na Ndoa.....

Picha
Leo nimeona nije hadharani hapa kutoa ushauri kwa mabinti wa makamo (30+yrs) ambao huenda kwa sababu za hapa na pale hawajafanikiwa kuingia kwenye ndoa wala kuwa na mahusiano yanayoashiria kuanzisha familia hivi karibuni. Msingi wa mada yangu umetokana na mabinti kadhaa ninao kutana nao mara kwa mara maeneo mbali mbali kuwa na vilio karibu sawa. Wakati nafanya kazi Taasisi fulani Dsm, kuna dada nilizoena nae kiasi cha kunisimulia baadhi ya mikasa ya kimahusiano na changamoto anazopitia. Binti huyo mwenye miaka zaidi ya 30 alipitia magumu ikiwa ni pamoja na kutoa mimba kadhaa baada ya kutoona mwelekeo wa waliompachika, kuamua kugharamia mahusiano kwa kumuhudumia kila kitu mwanaume, kulazimika kubadili dini mara kadhaa kwa ajili ya mwanaume Ki uficho bila wazazi wala ndugu zake kujua. Yote hayo aliyafanya ili kuwaridhisha wanaume angalau aitwe Mke wa fulani!! Lakini cha ajabu alikuwa anaambulia patupu Si huyo tu, wako wengi wa namna hiyo na ambao wa...

Jay Dee Atiwa Hatiani, Atakiwa Amuombe Radhi Ruge wa Clouds FM

Picha
Mahakama ya Wilaya Kinondoni imemtia hatiani mwanamuziki nyota wa kike nchini Judith Wambura (Lady Jay Dee) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.Tokeo la picha la lady jaydee Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye "coverage" pana nchini kote na ikiwezekana duniani. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili. Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jay Dee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.

undani wa Msichana huyu Aliyebakwa Hadi Kufa – Makumira University

Picha
Mapema jana zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha). Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya Leo akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo. Hata hivyo Amenithibitishia kwamba Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai. Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo. Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.

Taarifa Kutoka Ikulu: Rais Magufuli na Rais Kenyatta Wazindua Barabara ya Southern By-pass

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016 wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya. Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi. Akizungumza katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi. Rais Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini nchi za Afrika Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa ...