RAY ABANWA KUHUSU MTOTO WA JOHARI, AFUNGUKA KUWA
SIKU chache baada ya kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi kuwa staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba na kuzaa kwa siri huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray kufunguka kuwa hahusiki kwa lolote. Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’. Hivi karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo aliweka wazi. Awali, Ray alisema si busara wala hataki... kuzungumza mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha. Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane...