Kusitishwa vikao vya bunge Uingereza kwazua hasira kali
Uamuzi wa waziri mkuu kusitisha bunge umesababisha ghadhabu kutoka kwa wabunge na wapinzani wanaopinga kuidhinishwa Brexit bila mpangilio. Hatua hiyo ilichangia kuzuka maandamano kote nchini, kesi iliowasilishwa dhidi ya hatua hiyo na waraka uliosainiwa na zaidi ya watu milioni moja kupinga hatua hiyo. Serikali imesema kuistishwa kwa wiki tano kwa vikao vya bunge mwezi Septemba na Oktoba kutaruhusu muda wa kutosha kujadili Brexit. lakini wakosoaji wanasema ni hatua "isio ya kidemokrasi " kuwazuia wabunge kupinga brexit bila ya mpangilio. Waziri Michael Gove ameiambia BBC kwamba kusitishwa huko kwa bunge kulikoidhinishwa na Malkia siku ya Jumatano 'bila shaka sio' hatua ya kisiasa kuzuia upinzani kwa hatua ya Uingereza kujitoa katika Muungano wa Ulaya pasi kuwepo mpangilio. Ameeleza kwamba kutakuwa na "muda mwingi" kujadili Brexit kabla ya muda ulioorodheshwa wa kuondoka Oktoba 31. Hapo jana Jumatano Bwana Johnson alisema hotuba ya ...