Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2016

Sergio Ramos alivyozuia rekodi ya Real Madrid isivunjwe na FC Barcelona Dec 3 2016

Picha
Baada ya presha na ubishi wa zaidi ya wiki moja wa mashabiki wa FC Barcelona na Real Madrid za Hispania , kubishana timu ipi itapata ushindi katika mchezo wa El Clasico uliochezwa katika uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona , hatimae ubishi umemalizwa usiku wa December 3 2016. Timu za Barcelona na Real Madrid zote ziliingia zikiwa na kumbukumbu kuwa mchezo wao wa mara ya mwisho kumalizika pasipo goli ilikuwa ni mwaka 2002, huku Real Madrid waliingia kutetea rekodi yao ya kucheza mechi yao ya 33 bila kuruhusu kupoteza mchezo hata mmoja na kutoka sare mechi 6 pekee. December 3 2016 katika uwanja wa Nou Camp mchezo huo wa El Clasico umemalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, FC Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa Luis Suarez na Real Madrid wakafanikiwa kusawazisha goli dakika ya 90 kupitia kwa Sergio Ramos . Msimamo wa LaLiga baada ya matokeo ya mechi ya FC Barcelona ...

MAMBO Yanayoshusha Thamani ya Mwanaume Mbele ya Mwanamke

Picha
Katika uhusiano baina ya mume na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu. Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele ya mwanamke. Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele ye mwanamke: 1. HADAA NA UNYONYAJI: Baadhi ya wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha mapenzi. Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu matatizo ya kipesa na kiuchumi. Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo. 2. WANAWAKE WENGI: Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume. Kuwa na uhusiano na wana...

BONGO Movie Yazidi Kufa, JB Nae Aacha Kuigiza

Picha
Msanii wa siku nyingi wa bongo movie JB amestaafu kuigiza bongo movie, hii imesikitisha sana wadau wa sanaa, kuanzia mashabiki hadi wasanii wenzake..

TAHARUKI...Panya Road Wavamia Nyumba na Kupora..Majirani Washindwa Kusaidia

Picha
DAR: Kundi kubwa la vijana wanaosadikika kuwa ni 'Panya Road' wavamia nyumba moja na kupora vitu mbalimbali usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa kuwa mhanga wa tukio hilo alijaribu kuomba msaada kwa majirani bila mafanikio kwakuwa majirani hao waliogopa kutoka na kupambana na Panya Road hao. Mmoja wa majirani amenukuliwa akisema kuwa Vijana hao walikuwa na Mapanga Marungu, Jambia na Baruti walizokuwa wakizilipua ili kutisha watu kuwa ni Risasi.