Sentensi 12 za MPOKI kuhusu msiba wa Kapteni John KOMBA.. #RIP John Komba
                  Msanii wa Kundi la Orijino Komedi , Mujuni Sylivery  aka  Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya  uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA  ambaye amefariki siku ya juzi February 28.    Leo Mpoki amesikika kwenye Leo Tena @CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “ ..Mtu  akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu  unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda  Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu  yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu ”    “ Imeniathiri  kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini  ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga  mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa  wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo.. “    “ mwisho  wa siku kaondoka pengo lake halitozibika...